• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pande zinazopingana nchini Sudan Kusini zaahirisha kusaini makubaliano ya amani

    (GMT+08:00) 2018-07-20 19:05:18

    Pande zinazopingana nchini Sudan Kusini zimeahirisha kusaini makubaliano ya awali ya kugawana madaraka.

    Waziri wa habari wa Sudan Kusini Michael Makuei amesema, pande hizo zilizokuwa zinafanya majadiliano nchini Sudan, zimeshindwa kufikia mwafaka kuhusu masuala muhimu ambayo yanapaswa kutatuliwa kabla ya kusaini makubaliano. Amesema kutokana na hilo, ujumbe wa serikali umerejea mjini Juba kujadiliana na uongozi na serikali ili kuweza kupata kauli ya mwisho kuhusu masuala hayo.

    Wakati huohuo, Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, wafanyakazi 10 wa mashirika ya kibinadamu wameuawa nchini Sudan Kusini tangu mwezi Januari mwaka huu kutokana na kuongezeka kwa vurugu nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako