• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gharama ya maisha kupanda

    (GMT+08:00) 2018-07-20 20:00:47

    Gharama ya maisha nchini Kenya inatarajiwa kupanda zaidi kuanzia katika muda siku 10 zijazo kutokana na ushuru mpya wa bidhaa. Kodi hiyo ni kando na iliyowekwa kwenye bajeti mwezi uliopita.

    Ushuru huo mpya unahusu bidhaa kama maji, sharubati, pikipiki na marupurupu ya wafanyakazi. Wanywaji pombe pia wataumia kwani vileo pia vitapanda bei.

    Hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi mwezi Septemba wakati bidhaa za mafuta zitakapoanza kutozwa ushuru mpya wa ziada (VAT). Hii ni kutokana na kuwa ongezeko la bei za mafuta husababisha kupanda kwa bei za bidhaa za kimsingi kutokana na gharama za usafirishaji bidhaa.

    Kwa sasa, bei ya petroli ni Sh113 kwa lita jijini Nairobi na viunga vyake na inatazamiwa kuongezeka hadi Sh130 kuanzia Septemba. Hii inamaanisha kuwa bei za unga, sukari, usafiri miongoni mwa zingine pia zitapanda wauzaji wakipitisha gharama kwa wanunuzi.

    Kulingana na kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PwC), KRA haikuongeza kodi ya bidhaa za mafuta kwenye bajeti ya Juni kwa sababu ya ushuru mpya wa VAT kwa bidhaa za mafuta utakaonza kutumika Septemba.

    Kwenye mwongozo wa ushuru ambao KRA ilichapisha Ijumaa wiki jana, Wakenya watakuwa wakitozwa ushuru mpya wa moja kwa moja wanaponunua maji ya chupa, sharubati na mjazo wa simu kuanzia Agosti.

    Kwa mara ya kwanza, KRA itaanza kutoza ushuru mpya wa asilimia 5.2 kwa bidhaa hizi jambo ambalo shirika hilo linasema ni kuepusha serikali na athari za kupanda kwa gharama ya maisha.

    Katika mwongozo huo mpya, ushuru wa lita moja ya sharubati ya matunda utaongezeka kutoka Sh10 hadi Sh10.5 nao wa maji utapanda kutoka Sh5 hadi Sh5.2 kwa lita. Watengenezaji wa bidhaa hizi watapitisha gharama hiyo kwa wateja kwa kupandisha bei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako