• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na UAE zakubaliana kuinua uhusiano wao na kuwa ushirikiano wa kina wa kimkakati

    (GMT+08:00) 2018-07-21 09:14:57

    China na Umoja wa Falme za Kiarabu UAE jana ziliamua kuboresha uhusiano wao wa pande mbili na kuwa ushirikiano wa kina wa kimkakati.

    Uamuzi huo umefikiwa wakati rais Xi Jinping wa China ambaye yuko ziarani katika Umoja wa Falme za Kiarabu, alipofanya mazungumzo na Makamu wa rais ambaye pia ni Waziri mkuu wa UAE Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum na Mrithi wa kiti cha mfalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan.

    Kwa kuinua ushirikiano wao, China na Umoja wa Falme za Kiarabu zitaimarisha uhusiano wa kina kwenye Nyanja tofauti, na kukuza maendeleo endelevu ya uhusiano huo na kuwa wa ngazi ya juu, kwenye maeneo mapana zaidi na kina kikubwa.

    Akikumbishia mkutano wake na Mrithi wa kiti cha Mfalme mwaka 2015 wakati pande mbili zilipofikia makubaliano mengi muhimu katika kuendeleza ushirikiano wa kirafiki wa pande mbili, amesema uhusiano huo umeingia katika hatua mpya ya maendeleo ambayo ni ya kina na ya kasi, na kusisitiza kuwa ushirikiano huu una matarajio mazuri na uwezekano mkubwa.

    Katika mazungumzo hayo Makamu wa rais ambaye pia ni waziri mkuu Sheikh Mohammed bin Rashid Al Makhtoum amesema UAE imependezwa na maendeleo na mafanikio ya China, na kukubali utekelezaji wake wa mkakati wa maendeleo ya kufungua mlango, na kuongeza kuwa nchi yake iko tayari kuendeleza ushirikiano wa karibu na China katika maeneo mbalimbali na kuwa rafiki wa kutemegewa na China.

    Kwa upande wake Mrithi wa kiti cha mfalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan amesema nchi yake inakubaliana na wazo na mtazamo wa rais Xi katika utawala, na kusema anaamini China itakuwa na mustakabali mzuri na kutoa mchango mkubwa katika amani na maendeleo ya binadamu duniani.

    Rais Xi yupo Umoja wa Falme za Kiarabu katika ziara yake rasmi ambayo ni ya kwanza kwa rais wa China katika miaka 29 iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako