• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Maendeleo ya China yatoa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 50 kwa nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-21 09:56:03

    Msemaji wa Benki ya Maendeleo ya China (CDB) ambaye pia ni mchumi mkuu Bw. Liu Yong amesema kuwa benki hiyo imetoa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 50 kwa uwekezaji wa miradi karibu 500 katika nchi 43 za Afrika.

    Bw. Liu amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari, na kuongeza kwamba benki hiyo inaunga mkono ujenzi wa miradi muhimu katika nchi za Afrika kwa kutoa fedha nyingi za muda mrefu, jambo ambalo limeendeleza kwa ufanisi sekta za miundombinu, nishati, madini, mawasiliano ya simu, uzalishaji viwandani, na mambo ya kijamii katika nchi hizo.

    Pia amesema hatua ifuatayo ni kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, na kuendeleza ushirikiano kati ya pande hizo mbili hadi kwenye ngazi ya juu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako