• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Jubilee wa Kenya asema China kamwe haitafanya ukoloni barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-21 10:17:47

    Katibu mkuu wa chama tawala cha Kenya Jubilee Bw. Raphael Tuju amekanusha lawama kuwa China inafanya "ukoloni mambo leo" barani Afrika. Amesema China haikuwa na koloni lolote tangu zamani, hivyo hakuna msingi wowote kwa kulaumiwa kufanya ukoloni nchini Kenya pamoja na nchi nyingine barani Afrika.

    Bw. Tuju amesema ingawa kuna tofauti kati ya China na Kenya katika mambo ya utamaduni na dini, lakini mioyo kati ya watu wa nchi hizo mbili inaungana, ndiyo maana nchi hizo mbili zinaweza kushirikiana.

    Kuhusu mafanikio makubwa iliyopata China katika miaka 40 iliyopita, Bw. Tuju amesema hakuna nchi nyingine yoyote inayoweza kupata mafanikio kama hayo katika muda huo mfupi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako