• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hotuba ya waziri mkuu wa China yaonyesha uchumi wa China unaendelea vizuri

    (GMT+08:00) 2018-09-21 17:57:36

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, hotuba iliyotolewa na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang kwenye ufunguzi wa mkutano wa 12 wa baraza la majira ya joto la Davos imetoa pendekezo jipya la kukuza nguvu mpya za kuendeleza uchumi wa dunia kwenye mageuzi mapya ya kiviwanda.

    Bw. Geng Shuang amesema, hotuba ya Bw. Li Keqiang imeonyesha kuwa, China inalinda kithabiti utandawazi wa uchumi duniani, uchumi wa China umeendelezwa vizuri, na China itaendelea kuhimiza mageuzi na kufungua mlango. Amesema kuwa, wajumbe wanaohudhuria mkutano huo wamesema wanapenda kushirikiana na China kunufaika na fursa ya maendeleo ya China, na kutimiza kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako