• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge waapa kuangusha pendekezo la ushuru wa mafuta

    (GMT+08:00) 2018-09-21 20:36:02

    Wabunge wameendelea kupinga pendekezo la Rais Uhuru Kenyatta la kutaka mafuta yatozwe ushuru wa ziada ya thamani (VAT) ya kima cha asilimia 8, wakisema ushuru huo utawaumiza zaidi Wakenya wanaozongwa na mzigo mzito wa gharama ya maisha.

    Wabunge hao kutoka mirengo ya Jubilee na NASA walisusia mikutano iliyoitwa na viongozi wao ili kuwashawishi kuunga mkono suala hilo pamoja na kupunguzwa kwa bajeti za bunge na hazina ya maendeleo katika maeneo bunge (CDF).

    Baadhi ya wabunge walisema wanamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta kuhusiana na ajenda zingine muhimu kama vita dhidi ya ufisadi anapinga vikali ushuru wa VAT kwa bidhaa za mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako