• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama lasisitiza umuhimu wa kuboresha uongozi na uwajibikaji katika shughuli za kulinda Amani

    (GMT+08:00) 2018-09-22 16:39:54

    Baraza la Usalama jana limetoa azimio ambalo linalenga kuboresha utendaji wa maofisa wa ngazi zote za shughuli za kulinda amani, litakaloboresha zaidi uongozi na uwajibikaji.

    Pendekezo la Azimio hilo namba 2436 liliwasilishwa kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa ili kuhakikisha viongozi wa shughuli za kulinda Amani wanakuwa na uwezo na uwajibikaji.

    Baraza hilo pia, limeeleza kusikitishwa na tuhuma za uhalifu na unyanyasaji wa kingono wakati wa shughuli za kulinda Amani na likiahidi kuunga mkono sera ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa ya kutovumilia aina yoyote ya makosa ya unyanyasaji wa kingono.

    Kwenye baraza hilo, wajumbe walibadilishana maoni na naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao, ambaye alisisitiza kuwa ili kuongeza ufanisi wa shughuli za kulinda usalama yafaa kuwepo ushirikiano na umoja kati ya nchi zinazochangia vikosi vya kulinda Amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako