• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukuta wa Mirerani umeleta faida (Kwa hisani ya gazeti la Nipashe)

    (GMT+08:00) 2018-11-16 20:14:54

    Baada ya kujenga ukuta wa Mirerani mkoani Manyara ili kuzuai wizi wa madini kutoka kwenye migodi ya Tazanite, sasa faida imeanza kushuhudiwa. Kwa sasa mapato kutoka kwenye migodi ya Tanzanite imepanda kutoka shilingi milioni 402 miezi kumi iliyopita, hadi shilingi bilioni 2.1.

    Haya ni kwa mujibu wa mkuu wa mko wa Manyara Alexander Mnyeti alipokuwa akisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa huo kwa makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan ambaye yuko huko kwa ziara ya kikazi. Baadhi ya madini yanayopatikana kwenye migodi ya Mirerani ni Tanzanite, Tsavorite, Toummaline, Rhodolite miongoni mwa madini mengine. Mkuu wa mkoa amepongezwa na makamu wa rais kwa juhudi zake za kuhakikisha kuwa mapato ya madini yanaongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako