• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China ahutubia mkutano wa kilele wa viongozi wa viwanda na biashara wa APEC

    (GMT+08:00) 2018-11-17 18:37:35

    Rais Xi Jinping wa China leo amehutubia mkutano wa kilele wa viongozi wa viwanda na biashara wa APEC, na kuitetea China juu ya namna inavyoshika mwelekeo sahihi wa maendeleo ya uchumi wa dunia, na kupata wazo la usimamizi wenye ufanisi kwa jumuiya ya kimataifa.

    Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, ni lazima kushikilia kufungua mlango, kujiendeleza, ushirikiano shirikishi, uvumbuzi wenye utaratibu, aidha kupinga kithabiti kujilinda kibiashara, hali ya upande mmoja, kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi wa WTO, kuufanya utandawazi wa kiuchumi uendelezwe kwa upande wa kufungua mlango zaidi, kuwanufaisha watu wengi zaidi, na uwe na uwiano na kunufaishana.

    Pia amesema, wakati China inapotimiza maendeleo yake yenyewe, inatoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya ustawi wa pamoja wa nchi mbalimbali duniani. Kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ni njia ya China ya kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja na dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako