Akiongea kwenye mkutano wa pembeni kwenye mkutano maalumu wa kilele wa 11 wa Umoja wa Afrika, Rais Kagame amesema mfuko huo utakuwa na bajeti ya kuanzia dola milioni 100 za kimarekani, na mpaka sasa nchi za Afrika zimechangia dola milioni 60 za kimarekani. Rais Kagame amezishukuru nchi 42 wanachama wa AU zilizotoa mchango, na kuzitaka nyingine 12 ambazo bado hazijatoa zifanye hivyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |