Rais Xi Jinping ametoa mwito wa kuendelea na mafungamano ya kikanda, kujenga uchumi ulio wazi wa Asia na Pasifiki, kuendelea kuhimiza uchumi kwa uvumbuzi na kuandaa nguvu mpya za ongezeko la uchumi, kushikilia kukamilisha mtandao wa mawasiliano na kuhimiza maendeleo shirikishi, na kushikilia kuzidisha uhusiano wa kiwenzi na kushirikiana kukabiliana na mchakato za pamoja.
Pia amesema, viongozi wa sehemu ya Asia na Pasifiki wana jukumu la kupanga mustakabali wa ushirikiano baada ya mwaka 2020 wa APEC. China itashiriki kwa kina kwenye mchakato wa ushirikiano wa APEC, kutoa mchango mpya kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya sehemu hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |