• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano maalumu wa kilele wa 11 wa AU wafuatilia suala la mageuzi ya Umoja huo

    (GMT+08:00) 2018-11-18 17:01:01

    Mkutano maalumu wa kilele wa 11 wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa, unafuatilia suala la mageuzi ya Umoja huo. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, mwenyekiti wa zamu wa Umoja huo rais wa Rwanda Bw. Paul Kagame, amesema lengo la mkutano huo ni kuhimiza mageuzi ya Umoja wa Afrika, na mageuzi hayo yakiwemo namna ya kuifanya kamati ya Umoja wa Afrika ifanye kazi kwa ufanisi, yanaweza kuifanya Afrika iwe bora zaidi, na kuwaletea Waafrika mustakbali wanaotaka.

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed amesema kiini cha mageuzi ya Umoja wa Afrika ni kujitegemea kifedha, na viongozi wa Afrika wanatakiwa kueleza wazi zaidi ahadi za kisiasa katika suala hilo.

    Wakati huohuo Rais Kagame amelishukuru Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo dhidi ya Eritrea, na kuwapongeza waziri mkuu Abiy Ahmed wa Ethiopia na Rais Isaias Afwerki wa Eritrea na wengine wanaoshirikiana na viongozi hao wawili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako