• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani na Korea Kusini wajadili suala la Korea Kaskazini kwa njia ya simu

    (GMT+08:00) 2019-01-22 09:35:38

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo jumapili alifanya mazungumzo na mwenzake wa Korea Kusini Bw. Kang Kyung-wha kwa njia ya simu, ambapo walijadili mipango yao kuhusu Korea Kaskazini.

    Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili pia wamesisitiza ahadi ya ushirikiano kati ya nchi zao.

    Siku hiyo Bw. Pompeo pia alifanya mazungumzo na mwenzake wa Japan Bw. Taro Kono kwa njia ya simu, ambapo walithibitisha lengo la kutokuwepo kwa silaha za nyukilia kwenye peninsula ya Korea.

    Ikulu ya Marekani Ijumaa iliyopita ilitangaza kuwa mkutano wa pili kati ya rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-Un utafanyika mwishioni mwa mwezi Februari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako