• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China asisitiza kuongeza uwezo wa kukabiliana na changamoto

    (GMT+08:00) 2019-01-22 10:16:25

    Mkutano wa wakuu wa ngazi ya mkoa na wizara wa Chama cha Kikomunisti cha China umeanza jana. Maudhui yake ni kushikilia wazo thabiti katika kukinga na kukabiliana na changamoto kubwa. Kwenye mkutano huo rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, inapaswa kutambua kihalisi mabadiliko makubwa yanayotokea nje, na changamoto zinazokabili maendeleo ya mageuzi ya China, kuongeza wazo la kukabiliana na hatari, na uwezo wa kukinga na kudhibiti, ili kujiepusha na hatari kubwa, na kuhakikisha hali ya uchumi na jamii inapata maendeleo endelevu na kwa hatua madhubuti.

    Katika hotuba yake, rais Xi amefafanua kwa kina maagizo katika kukinga na kukabiliana na changamoto zitakazozikabili nyanja za siasa, fikra, uchumi, sayansi na teknolojia, jamii, mazingira ya nje na ujenzi wa chama. Anasema:

    "Ili kukabiliana na hali yenye utatanishi ya kimataifa na mazingira yenye utata, pamoja na majukumu magumu ya kuhakikisha mageuzi, maendeleo na utulivu wa nchi, tunapaswa kudumisha tahadhari ya hali ya juu, ili kuepusha hatari zinazotabirika, na kukabiliana na zile zisizotabirika. Tunapaswa kuwa tayari kujikinga dhidi ya hatari hizo, na pia tunapaswa kuwa na uwezo wa kukabiliana nazo endapo zikitokea."

    Pia ameeleza kuwa, kamati ya chama na serikali kwenye ngazi mbalimbali zinatakiwa kutekeleza kithabiti mtizamo wa jumla wa usalama, kutekeleza maagizo mbalimbali ya kamati kuu katika kulinda usalama wa kisiasa, ili kuhakikisha usalama wa kisiasa. Vilevile amesisitiza kuwa, hali ya jumla ya uchumi kwa sasa nchini China ni nzuri, lakini maendeleo ya uchumi yanakabiliwa na mabadiliko makubwa tena yenye utatanishi ndani na nje ya nchi. Anasema:

    "Inapaswa kushughulikia vizuri uhusiano kati ya ongezeko lenye utulivu la uchumi na kujikinga dhidi ya hatari, kutekeleza ipasavyo mipango yenye ufanisi ya kuhakikisha soko la mali zisizohamishika linapata maendeleo kwa hatua madhubuti, kuimarisha utafiti na usimamizi wa soko na kuondoa mzizi wa hatari. Vilevile inapaswa kutatua kihalisi matatizo mbalimbali yanayovikabili viwanda vidogo na vyenye ukubwa wa kati."

    Mbali na hayo rais Xi pia amesisitiza kuimarisha uwezo wa ujenzi wa kimfumo na uwezo na kukamilisha utaratibu wa kufanya uvumbuzi, kushughulikia vizuri masuala yanayohusu maslahi ya wananchi, na kupambana kithabiti na ufisadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako