• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa dunia kuongezeka kwa asilimia 3 katika mwaka huu na mwaka kesho

    (GMT+08:00) 2019-01-22 18:48:39

    Ripoti ya mustakabali wa uchumi wa dunia wa mwaka 2019 iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imekadiria kuwa, uchumi wa dunia utaongezeka kwa asilimia 3 katika mwaka 2019 na mwaka 2020.

    Ripoti hiyo imeonesha kuwa, kutokana na kupungua kwa nguvu ya kuhimiza uchumi katika mwaka 2018, ongezeko la uchumi la Marekani litapungua hadi asilimia 2.5 mwaka 2019, na kufikia asilimia 2 katika mwaka 2020?. Ingawa kuna tishio la kupungua kwa ongezeko, ikiwemo athari ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, uchumi wa Umoja wa Ulaya utaongezeka kwa asilimia 2 katika mwaka huu na mwaka kesho, huku uchumi wa China unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 6.3 katika mwaka 2019.

    Mtaalamu wa uchumi wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya maendeleo ya uchumi Bw. Elliott Harris amesema, mgogoro wa biashara, kiwango cha juu cha madeni na mabadiliko ya hali ya hewa yanaleta tishio kwa maendeleo ya uchumi, lakini nchi mbalimbali zinapaswa kushirikiana na kukabiliana na changamoto kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako