• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukuaji mzuri wa uchumi wa China wawashangaza watu waliokuwa na shaka juu ya uchumi wa China

    (GMT+08:00) 2019-03-11 20:31:11

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang alitangaza vipimo 36 muhimu vya uchumi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la China mwaka jana, akiwakilisha baraza la serikali kutoa ripoti ya kazi ya serikali. Hii leo, serikali ya China imetangaza kuwa majukumu hayo yote yametimizwa.

    Maendeleo hayo yamekuwa pigo kubwa kwa watu waliokuwa na shaka juu ya uchumi wa China kutokana na kukabiliwa na migogoro mbalimbali ya kibiashara, na shinikizo la kushuka kwa uchumi.

    Kutokana na takwimu zilizotolewa na tovuti ya serikali ya China, ongezeko la pato la taifa la China GDP, bei ya matumizi ya fedha ya wakazi, ongezeko la idadi ya watu wanaopata ajira mijini na vijijini zote zimefikia vipimo vilivyowekwa. Ongezeko hilo linalingana na makadirio ya mashirika mengi yenye ushawishi mkubwa duniani. Mwaka 2018 Shirika la Fedha la Kimataifa IMF lilikadiria kuwa ongezeko la uchumi wa China litafikia asilimia 6.6, makadirio ya Benki ya Dunia ni asilimia 6.5, na Shirika la Ushirikiano na Maendeleo ya Uchumi lilikadiria kuwa ni asilimia 6.7.

    Mbali na takwimu hizo, kiwango cha maisha ya wananchi wa China kinaweza kuonesha kihalisi hali ya uchumi katika mwaka uliopita. Thamani ya viwanda vya bidhaa ya rejareja na vyakula iliongezeka kwa asilimia 8.5, idadi ya watalii kote nchini iliongezeka kwa asilimia 7.6, na pato linalotokana na utalii liliongezeka kwa asilimia 8.2.

    Mwaka 2018, China ilitimiza miaka ya 40 tangu ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufungaji mlango, maendeleo hayo ni kumbukumu nzuri zaidi kwa ajili ya maadhimisho hayo.

    Mikutano miwili ya mwaka huu itafanyika hivi karibuni, ambapo serikali ya China itatangaza mipango mipya ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, inakadiriwa kuwa, wananchi wa China watanufaika na mustakabali mzuri zaidi pamoja na dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako