• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa nne wa Mazingira wa UM wapitisha mipango ya kivumbuzi kukabiliana na changamoto zinazokabili mazingira

    (GMT+08:00) 2019-03-12 17:06:40

    Mkutano wa nne wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa umefunguliwa jana mjini Nairobi, Kenya. Wakati wa mkutano wa siku tano, wajumbe zaidi ya 4,700 kutoka nchi na sehemu 170 duniani wanatafuta teknolojia na njia mbalimbali za kutatua masuala ya mazingira, na kutimiza matumizi na uzalishaji endelevu.

    Mkutano huo ambao ni wa ngazi ya juu zaidi duniani, umewashirikisha watu zaidi ya 4,700 duniani wakiwemo viongozi wa serikali, mawaziri wa mazingira, maofisa wakurugenzi wa makampuni ya kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali, pamoja na wanaharakati wa mazingira. Maudhui yake kwa mwaka huu ni kutafuta njia za kivumbuzi katika kukabiliana na changamoto za mazingira na kutimiza matumizi na uzalishaji endelevu. Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni waziri wa mazingira wa Estonia Bw. Siim Kiisler, anasema:

    "Mkutano huu utaweka mkazo katika namna ya kufanya matumizi na uzalishaji kwa njia endelevu, na kutafuta njia za kivumbuzi. Katika miaka minne iliyopita, dunia imeshuhudia maafa mbalimbali yakiwemo mafuriko makubwa na ukame, ambavyo vimesababisha vifo vingi vya watu. Endapo hatutachukua hatua mara moja hatutaweza kubadilisha mwelekeo huu, na kulinda usalama wa binadamu na mazingira ya asili, pamoja na utaratibu wa dunia."

    Maamuzi yatakayopitishwa kwenye mkutano huo yataathiri kwa kina utekelezaji wa Makubaliano ya Paris na Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030, na kuondoa vikwazo kwa Mkutano wa kilele wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa ya Umoja wa Mataifa wa mwaka huu. Kaimu mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa Bibi Joyce Msuya anasema:

    "Kwanza tunapaswa kuchukua hatua haraka ili kupunguza utoaji wa hewa za Kaboni Dioxide, na kuendeleza uchumi usio na uchafuzi wa mazingira. Pili tutafikiria namna ya kupunguza athari mbaya zinazoletwa na uzalishaji wa vyakula kwa mazingira. Tatu tutatimiza kuondoa matumizi ya ovyo, na kuufanya uchumi wa mzunguko kuwa msukomo katika siku za baadaye."

    Naibu mkuu wa Chuo cha mazingira na maendeleo endelevu cha Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Chuo Kikuu cha Tongji cha China Bw. Li Fengting anasema:

    "China siku zote inajihusisha katika ushirikiano wa Kusini Kusini, ushirikiano na Afrika, na Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na uzoefu wake mwingi unaweza kuigwa na nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea. Tunatumai kueneza teknolojia zenye ufanisi na zisizo na uchafuzi wa mazingira katika nchi nyingine duniani."

    Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, wajumbe walifanya maombolezo ya kukaa kimya kuwakumbuka marehemu wa ajali ya ndege ya Ethiopia iliyotokea tarehe 10 Machi, ambao walikuwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, na wanasayansi wenye uzoefu mkubwa ambao walikuwa wanaenda kuhudhuria mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako