• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 40 wauawa katika shambulizi la kigaidi nchini New Zealand

    (GMT+08:00) 2019-03-15 18:40:19

    Waziri mkuu wa New Zealand Bi. Jacinda Ardern leo amesema, watu 40 wameuawa na wengine 27 kujeruhiwa katika shambulizi la ufyatuaji risasi lililotokea leo katika misikiti miwili mjini Christchurch nchini humo.

    Bi. Ardern amethibitisha kuwa shambulizi hilo ni la kigaidi, na kuongeza kuwa shambulizi hilo lilipangwa kwa muda mrefu. Mabomu mawili yaliyotegwa kwenye magari yameteguliwa na kuondolewa na polisi. Ameongeza kuwa watu wanne wamekamatwa, huku watatu wakituhumiwa kuhusika na shambulizi hilo, akiwemo mzaliwa wa Austria mwenye itikadi kali.

    Bi Jacinda amesema hali ya usalama nchini kote imeimarishwa hivi sasa.

    Washambuliaji wasiopungua wawili wenye silaha wamefyatua risasi leo ndani ya misikiti miwili tofauti yenye watu wengi mjini Christchurch.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako