• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti yaonesha kuwa ushawishi wa China duniani umezidi wa Marekani

    (GMT+08:00) 2019-03-15 18:51:04

    Ripoti mpya ya uchunguzi wa maoni iliyotolewa na kampuni ya Gallup ya Marekani imeonesha kuwa, kiwango cha uungaji mkono wa uongozi wa China duniani kimekuwa asilimia 34, huku kiwango hicho cha Marekani kikiwa asilimia 31. Hii ni mara nyingine kwa uongozi wa China duniani kuzidi wa Marekani tangu msukosuko wa fedha duniani utokee mwaka 2008.

    Uchunguzi huo unaohusiana na uwezo wa uongozi wa China, Marekani, Russia na Ujerumani duniani umefanywa katika nchi na sehemu 134 kote duniani. Ripoti hiyo pia imeonesha kuwa barani Ulaya, Asia na Afrika, kiwango cha kuitambua China kuwa kiongozi wa duniani kimezidi cha Marekani, na kiwango hicho ni cha juu zaidi barani Afrika ambacho kimefikia asilimia 53.

    Kama tunavyofahamu, kutokana na mgogoro wa mikopo ya kibinafsi wa Marekani, mwaka 2008 uchumi wa dunia uliathiriwa vibaya na mgogoro huo. China ilikuwa nguvu kuu ya kuokoa uchumi wa dunia na kuhimiza ongezeko la uchumi huo. Uchunguzi uliofanywa na kampuni ya Gallup mwaka 2008 ulithibitisha kwa mara ya kwanza ushawishi wa China duniani umezidi Marekani.

    Miaka kumi imepita, kutokana na maendeleo ya uchumi wa China, uchumi wa dunia umefufuka na kujitokeza na mwelekeo wa ukuaji. Lakini baadhi ya nchi za magharibi haziwezi kutatua matatizo ya ndani na kusababisha ongezeko la pengo kati ya tabaka la juu na la chini na ongezeko la madeni.

    Miaka ya hivi karibuni, China imejenga jukwaa kubwa zaidi la ushirikiano wa kunufaishana duniani, ambalo nchi 123 na mashirika 29 ya kimataifa yamesaini nyaraka za makubaliano ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na China. Pendekezo hilo limekuwa jukwaa linalopendwa zaidi na nchi mbalimbali duniani. Kama waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alivyosema, kutokana na utekelezaji wa miradi ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja", barabara kuu ya kwanza imejengwa kwenye Afrika Mashariki, Maldives imekuwa na daraja la kwaza la kuvuka bahari, Belarus imekuwa na kiwanda cha kwanza cha kutengenezea magari, na Kazakhstan imepata njia yake ya kwanza ya kuingia baharini.

    Ushahidi umethibitisha kuwa misimamo ya uhusiano mpya wa kimataifa na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja imekaribishwa na jumuiya ya kimataifa, na kuwa sehemu muhimu ya uongozi wa China kwa dunia.

    Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya Gallup Bw. Jon Clifton amesema, kama uchumi na nguvu ya kijeshi ya nchi moja inawakilisha nguvu ngumu ya nchi moja, na nguvu yake laini inaonekana kuwa nchi nyingine zinataka kuifuata nchi hiyo kwa hiari badala ya kulazimishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako