• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China kudumisha ukuaji imara

    (GMT+08:00) 2019-03-15 19:27:26

    Mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China umefungwa leo. Katika mustakabali ambao mashirika makuu ya kimataifa yamepunguza makadirio ya ongezeko la uchumi wa mwaka huu, mkutano huo umetangaza makadirio mazuri kuhusu ukuaji wa uchumi wa China, huku ukitoa mapendekezo na mipango ya kutimiza makadirio hayo.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesisitiza kuwa, uchumi wa China utaendelezwa kwa kiwango cha maana, na kuhakikisha maendeleo yenye ubora wa juu. Nguvu mpya inayoongozwa na uvumbuzi imekuwa chanzo kipya cha ukuaji wa uchumi wa China, ambayo sio tu itaendelea kuboresha maisha ya umma, bali pia italeta fursa za maendeleo yatakayoinufaisha dunia.

    Mkutano huo umetoa taarifa nzuri kadhaa za kunufaisha wananchi na mashirika na kuendelea kuboresha mazingira ya maendeleo ya China, ikiwa ni pamoja na sheria ya uwekezaji wa kigeni iliyopitishwa na bunge la umma la China. Sheria hii itasaidia kulinda maslahi halali za uwekezaji wa kigeni, kujenga mazingira ya kibiashara ya kisheria, kimataifa, kurahisisha mazingira ya kibiashara, kutekeleza hatua kubwa zaidi za kupunguza ushuru na kodi, kuzidi kurahisisha utaratibu na kuboresha huduma.

    Katika mchakato wa kuinua kiwango cha uchumi wa China na kutimiza maendeleo yenye ubora wa juu, umuhimu ni kuimarisha nguvu mpya ya kuhimiza maendeleo. Ripoti ya kazi za serikali ya mwaka huu imesema, nguvu mpya ya kuhimiza maendeleo inabadilisha kwa kina mitindo ya maisha na uzalishaji na kuunda msukumo bora mpya ya maendeleo ya China, huku ikipendekeza kuhimiza mkakati wa "Internet +" katika sekta mbalimbali na kutoa kwa mara ya kwanza dhana ya "Akili +". Ni dhahiri kwamba mtandao wa Internet, akili bandia na kuinua kiwango cha shughuli za jadi zitatoa mchango mkubwa zaidi katika kuhimiza maendeleo ya viwanda vinavyojitokeza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako