• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yakanusha ripoti ya wanafunzi wawili kuhukumiwa adhabu ya kifo nchini China

    (GMT+08:00) 2019-03-16 17:08:49

    Serikali ya Zambia jana ilikanusha ripoti zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba wanafunzi wawili wa raia wa nchi hiyo wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini China kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya.

    Wizara ya mambo ya nje ya Zambia imesema taarifa kama hizo ni za kughushi tu na ni lazima zipuuzwe.

    Balozi wa Zambia nchini China, Winnie Chibesakunda amesema ubalozi wake haujapokea adhabu kama hiyo au wala kurekodiwa na mamlaka za China, na kusisitiza kuwa hakuna wanafunzi wa Zambia nchini China wenye majina yaliyotajwa kwenye ripoti zinazosambaa mitandaoni. Ameeleza kuwa ubalozi mara zote unafuatilia mambo ya wanafuzi wote waliopo China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako