• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Ethiopia kuongoza ujumbe wa ngazi ya juu kwenye mkutano wa pili wa baraza la "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2019-03-16 18:54:05

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed amethibitisha kuhudhuria mkutano wa pili wa baraza la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" utakaofanyika mwezi ujao hapa Beijing.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Bw. Nebiat Getachew hivi karibuni amesema kuwa, Ethiopia ni mwenzi muhimu wa China barani Afrika. Kuhudhuria kwa Ethiopia katika mkutano huo kunathibitisha zaidi uhusiano imara kati ya nchi hizo mbili.

    Hivi karibuni, Ethiopia imeeleza nia yake ya kutekeleza makubaliano kati yake na China. Balozi wa Ethiopia nchini China Bw. Teshome Toga Chanaka ametoa mwito wa kushirikiana zaidi katika maeneo yanayotoa kipaumbele maslahi ya pamoja, likiwemo baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako