• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kufanya mkutano wa pili wa maendeleo ya kidijitali mwezi ujao

    (GMT+08:00) 2019-04-02 20:30:29

    Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imesema, China itafanya mkutano wa pili wa maendeleo ya kidijitali kuanzia tarehe 6 hadi 8 mwezi ujao mjini Fuzhou, mji mkuu wa mkoa wa Fujian.

    Naibu mkurugenzi wa Idara ya Mtandao wa Internet ya China Yang Xiaowei amesema, mkutano huo utatumika kama jukwaa la kutoa sera za China kuhusu maendeleo ya teknohama, kuonyesha mafanikio ya uongozi na uchumi wa kidijitali, pamoja na mabadilishano ya nadharia na kivitendo katika kujenga China ya kidijitali.

    Mkutano huo unaandaliwa kwa pamoja na Idara ya Mtandao wa Internet ya China, Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China, Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari, pamoja na serikali ya mkoa wa Fujian.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako