• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuchukua hatua tano kuhimiza ufunguaji mlango kwenye kiwango cha juu zaidi

    (GMT+08:00) 2019-04-27 11:18:49

    Rais Xi Jinping wa China akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Baraza la Ushirikiano wa Kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", amesisitiza kuwa inapaswa kusukuma mbele ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwenye kiwango chenye sifa ya juu, na kutangaza hatua tano muhimu zitakazochukuliwa na China katika kuhimiza ufunguaji mlango kwa kiwango cha juu zaidi.

    Hatua hizi zimeonesha kuwa China iliyo wazi zaidi si kama tu itahimiza ujenzi wenye sifa ya juu wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", bali pia utaleta fursa mpya kwa ukuaji wa uchumi duniani, na kukamilisha mambo ya usimamizi wa uchumi duniani.

    Hivi sasa ongezeko la uchumi duniani linakabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na kujilinda kibiashara na utaratibu wa upande mmoja unaoongezeka. "Ukanda Mmoja, Njia Moja" likiwa ni pendekezo la ushirikiano wa kiuchumi wa kimataifa, linalotafuta maendeleo yenye sifa ya juu, si kama tu linakidhi mahitaji katika kutimiza ongezeko la uchumi shirikishi duniani, bali pia linalingana na mahitaji ya ukuaji wa uchumi wa China unaoingia kwenye kipindi cha kupata maendeleo yenye sifa ya juu.

    Kipaumbele cha ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni mawasiliano. Kwenye hotuba yake, rais Xi Jinping ametangaza hatua tano ili kuhimiza kufungua mlango kwenye kiwango cha juu zaidi, hasa kuweka mipango kuhusu mambo ya kimfumo na kimuundo, hatua ambayo inafuata mahitaji ya maendeleo yenye sifa ya juu ya uchumi ya China, na kuonesha nia ya China ya kufungua mlango zaidi.

    Hatua hizo tano ni pamoja kwanza China itazidi kupunguza masharti ya kuwekeza kwa kampuni kutoka nje. Rais Xi ametangaza kuwa katika siku za baadaye China itaendelea kuhimiza ufunguaji mlango kwa pande zote katika sekta za utoaji wa huduma za kisasa, uzalishaji viwandani na kilimo, na kuidhinisha kampuni za kigeni kumiliki hisa na kujiendesha kwa kujitegemea katika maeneo mengi zaidi. Hatua ambayo itasaidia utekelezaji wa Sheria ya uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni iliyotangazwa hivi karibuni nchini China, ili kuweka mazingira yenye usawa ya ushindani kwa ajili ya kampuni zote zenye uwekezaji wa kigeni.

    Hatua ya pili ni kuongeza nguvu katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika ulinzi wa hakimiliki ya ubunifu. Rais Xi ametangaza kuwa China itakamilisha kwa pande zote utaratibu wa sheria kuhusu sekta hiyo, kuongeza ulinzi wa maslahi halali ya wamiliki hakimiliki wa nchi za nje, kupiga marufuku vitendo vya kulazimisha uuzaji wa teknolojia, na kupambana vikali na vitendo vya kukiuka hakimiliki ya ubunifu.

    Hatua ya tatu ni kuongeza uagizaji wa bidhaa na huduma kwa kiasi kikubwa zaidi. Rais Xi ameahidi kuwa China itazidi kupunguza kiwango cha ushuru wa forodha, kuondoa vikwazo mbalimbali visivyo vya ushuru wa forodha, kuingiza mazao ya kilimo yenye sifa bora, bidhaa na huduma kutoka nchi za nje ambazo zina uwezo mkubwa wa ushindani. Hatua hizo si kama tu zitakidhi kiwango cha matumizi cha wachina kinachoongezeka, bali pia zitahimiza maendeleo ya biashara yenye uwiano kati ya China na nchi mbalimbali duniani, ili kupanua soko kubwa zaidi kwa nchi mbalimbali nchini China.

    Hatua ya nne ni kutekeleza kwa ufanisi zaidi uratibu wa sera ya jumla ya uchumi ya kimataifa. Rais Xi amesisitiza kuwa China itaimarisha uratibu na makundi makubwa ya kiuchumi duniani kuhusu sera ya jumla, kutopunguza kiwango cha ubadilishaji wa fedha, kufanya juhudi za kuunga mkono na kushiriki kwenye mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani WTO, ili kuhimiza kufungua mlango kwa China kufikie kiwango cha juu zaidi.

    Hatua ya tano ni kuweka mkazo zaidi katika utekelezaji wa sera za ufunguaji mlango. Kwenye hotuba hiyo rais Xi amesisitiza kuwa China inatilia maanani katika utekelezaji wa makubaliano ya kiuchumi na kibiashara kati yake na nchi mbalimbali, kuanzisha utaratibu wa utekelezaji wa makubaliano hayo ya kimataifa, kurekebisha na kukamilisha sheria na kanuni kwa kufuata mahitaji ya upanuzi wa ufunguaji mlango.

    Hivi sasa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" likiwa pendekezo lililotolewa na China na kuhudumia dunia nzima, ujenzi wake uko katika kipindi muhimu cha utekelezaji halisi. Hatua za China za kuhimiza kufungua mlango kwenye kiwango cha juu zaidi zitaweka injini kubwa zaidi katika maendeleo yenye sifa ya juu zaidi ya ujenzi huo, na pia kutoa fursa nyingi zaidi kwa ajili ya mafungamamo ya kiuchumi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako