Watalii hao waliwasili katika hifadhi hiyo wakitokea kwa magari maalumu ya kitalii na kupokelewa kwa ngoma za asili za kabila la Kimasai na Watatoga.
Baada ya kuingia lango kuu la hifadhi walionekana wakiwa na furaha, huku baadhi yao wakionekana wakipiga picha msitu mnene waliouona na wanyama.
Aidha, walilazimika kushuka baadhi ya maeneo na kupiga picha kwenye miti mikubwa na magogo ya miti iliyolala.
Baadhi ya watalii hao walihudhuria kongamano la uwekezaji lililofanyika ukumbi wa kimataifa wa mikutano AICC uliopo Mjini Arusha, huku wenzao wakitangulia Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro.
Awali Mwenyekiti wa Kampuni ya Touchroard International Holdings Groups ya China, He Lei Hiu, alisema wamefurahishwa na ukarimu wa Watanzania na mapokezi makubwa waliopatiwa.
Alisema katika ziara hiyo, wameanza kwa kutembelea vivutio vya utalii vya Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro na kujionea wanyama wa kila aina waliowavutia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |