• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huawei yasema vikwazo dhidi yake haviwezi kuleta usalama zaidi kwa Marekani

    (GMT+08:00) 2019-05-16 19:50:46

    Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Huawei ya China imesema, vikwazo vilivyowekwa na Marekani haviwezi kuongeza usalama zaidi nchini humo, na vinaweza kuifanya nchi hiyo ishindwe na nchi nyingine katika ujenzi wa mtandao wa 5G.

    Kauli hiyo imekuja baada ya serikali ya Marekani jana kutangaza kuweka vikwazo dhidi ya baadhi ya kampuni ikiwemo kampuni ya Huawei ya China. Taarifa iliyotolewa na idara ya viwanda na usalama ya wizara ya biashara ya Marekani imesema, itaiorodhesha Huawei kwenye kampuni na watu binafsi ambavyo vinahitaji ruhusa ya serikali ya Marekani kabla ya kupata teknolojia za nchi hiyo.

    Huawei imesema kampuni hiyo ni mtangulizi katika sekta ya vifaa vya 5G, na inapenda kudumisha mawasiliano na serikali ya Marekani kuhusu hatua za kuhakikisha usalama. Endapo Marekani ikiiwekea vikwazo Huawei, italazimika kuagiza vifaa kwa bei ghali, na kudhuru maslahi ya kampuni na wateja wa nchi hiyo. Aidha, imesema vikwazo hivyo pia vitaiingiza Mareani kwenye matatizo ya kisheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako