• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China si adui wa kweli wa Marekani

    (GMT+08:00) 2019-05-16 20:40:30

    Hivi karibuni Steve Bannon aliyekuwa mshauri wa juu wa kimkakati wa rais wa Marekani alitunga makala ndefu, akisema China imekuwa adui mkuu wa Marekani, na kutaka serikali ya Marekani isirudi nyuma katika vita vya kiuchumi na China. Lakini Makala hiyo ikichambuliwa kwa undani, ni wazi kuwa haina msingi na mantiki sahihi. Wanasiasa wa mrengo wa kulia wanachochea migongano kati ya Marekani na nchi nyingine, na hao ndio maadui wa kweli wa Marekani.

    Kwenye makala yake, Bannon analaumu China kwa kufanya vita vya kiuchumi na nchi za kiviwanda na kidemokrasia. Lakini ukweli ni kwamba, pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limekuwa jukwaa la ushirikiano wa kiuchumi ambalo linakaribishwa zaidi na jumuiya ya kimataifa. Bannon ametoa tuhuma zisizo na msingi kuwa, China inaiba na kunyang'anya teknolojia za Marekani. Mwaka 2017, idadi ya maombi ya hataza ya China ilichukua nafasi ya kwanza duniani, na China imekuwa moja ya nchi yenye hakimiliki nyingi zaidi za kiubunifu, kamwe haina haja ya "kuiba" vitu vya nchi nyingine.

    Kwenye Mazungumzo ya Ustaarabu ya Asia yaliyoanza jana, rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa kusikilizana na nchi nyingine duniani ni desturi ya kijadi ya China. Jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja iliyopendekezwa na rais Xi inaonesha wazo la China la kushirikiana na nchi nyingi ili kupata maendeleo ya pamoja.

    Baadhi ya wabunge wa Marekani jana wamekabidhi mswada wa sheria kwa bunge la nchi hiyo, na kutaka kupiga marufuku kutoa visa kwa watu wanaofanya kazi katika idara za utafiti wa kijeshi za China, ili kupunguza hatari za usalama. Siku hiyo hiyo, ikulu ya Marekani imetangaza kupiga marufuku kampuni za nchi hiyo kutumia vifaa vya upashanaji habari vya kampuni zenye hatari, ambazo zinaaminiwa kuwa kampuni za China haswa Huawei.

    Wakati wa kuendelea kwa kasi kwa utandawazi wa uchumi, ni ajabu kwamba, Marekani, ambayo ni nchi yenye nguvu kubwa zaidi ya kiuchumi na kijeshi duniani, inataka kufunga mlango wake. lakini kusema kweli, anayeweza kuishinda Marekani ni nchi hiyo yenyewe, na wanasiasa wa mrengo wa kulia ni maadui kweli wa Marekani.

    Rais Xi alisema kujilinda kibiashara ni kama kujifungia kwenye chumba kisicho na mlango wala dirisha, inaweza kuepuka upepo na mvua, lakini pia itakosa mwanga wa jua na hewa bora. Hivi sasa kutokana na wanasiasa wa mrengo wa kulia, Marekani inajifungia kwenye chumba cha giza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako