• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yafikiria kutunga miongozo mipya juu ya kadi za chanjo ya homa ya manjano

    (GMT+08:00) 2019-05-17 09:40:48

    Wizara ya Afya ya Kenya inachukua hatua kurahisisha utoaji wa kadi za chanjo ya homa ya manjano katika vituo vya afya kwenye viwanja vya ndege nchini humo.

    Waziri wa Afya wa nchi hiyo Bibi Sicily Kariuki amesema hii inalenga kuanzisha hatua kali zaidi katika mchakato wa utoaji wa kadi hizo za chanjo ambayo itazuia ongezeko la kesi za kadi feki za chanjo ya homa ya manjano

    Bi Kariuki amesema kuna kesi nyingi zinazoongezeka kuhusu wasafiri kuchukua muda mrefu maeneo ya mpakani wakisubiri ruhusa kutokana na ukosefu wa chanjo au kuchukua kadi feki za chanjo ya homa ya manjano, na kwa wale waliotaka kwenda nchi za kigeni walipata hasara kubwa kwa kushindwa kufika maeneo wanayotaka kwenda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako