• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa kuunga mkono juhudi za Ethiopia kupitia mipango ya kimkakati na kitaalamu

    (GMT+08:00) 2019-05-17 09:44:12

    Umoja wa Mataifa umeapa kuunga mkono juhudi za serikali ya Ethiopia kupitia mipango ya kimkakati na kitaalamu hasa katika sekta ya fedha na maendeleo ya kidigitali.

    Ahadi hiyo ilitolewa na Malkia Maxima wa Uholanzi, ambaye pia ni mshauri maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia sera za fedha jumuishi kwa ajili ya maendeleo, wakati alipokutana na waziri wa fedha wa Ethiopia Bw. Ahmed Shade.

    Kwenye taarifa yake Bw. Shade amesema, Malkia Maxima ataunga mkono kwa njia ya kutuma wataalamu wenye ujuzi wa fedha na mipango.

    Malkia huyo ambaye yuko ziarani nchini Ethiopia ikiwa sehemu ya ziara yake ya siku tatu inayolenga kuhimiza upatikanaji wa huduma nchini humo, ametaka kuhimiza matumizi ya tekonolojia ya kidigitali katika huduma za fedha nchini Ethiopia pamoja na maendeleo ya mfumo wa kidigitali wa kitambulisho cha taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako