• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waeleza wasiwasi kuhusu kurejea tena kwa vurugu nchini Sudan

    (GMT+08:00) 2019-05-17 09:44:42

    Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake juu ya kurejea tena kwa hali ya wasiwasi nchini Sudan kati ya baraza la mpito la kijeshi TMC na viongozi wa maandamano.

    Alipoulizwa kuhusu hali nchini Sudan, msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, anaona ni muhimu kwa utawala kuweka kipaumbele katika mazungumzo ili kutatua tofauti zinazoweza kuwepo na vurugu za aina yoyote zinazoweza kuharibu usalama wa raia wote pamoja na utulivu wa nchi hiyo zinapaswa kuepushwa.

    Ameongeza kuwa ni muhimu kuheshimu haki za watu za kuandamana kwa njia ya amani. Aidha katibu mkuu wa Umoja huo Bw. Antonio Guterres amepongeza mchakato wa mazungumzo nchini Sudan na kuzitaka pande husika kudumisha mwelekeo mzuri na kufikia makubaliano katika masuala yaliyosalia ya kugawana madaraka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako