• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatua ya Marekani kupandisha migogoro ya biashara na China yaathiri vibaya mazungumzo kati ya pande mbili

    (GMT+08:00) 2019-05-17 10:03:16

    Msemaji wa Wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, China haifahamu mpango wa upande wa Marekani kuja China kufanya majadiliano, na kwamba hatua ya Marekani ya kupandisha migogoro ya biashara imeathiri vibaya mazungumzo ya biashara kati ya pande hizo mbili.

    Bw. Gao amesema China siku zote inaona kuwa hatua ya kuongeza ushuru wa forodha dhidi ya bidhaa za China zinazouzwa nchini Marekani haisaidii utatuzi wa migogoro ya biashara kati ya pande hizo mbili. Akisema kwamba China haitaki vita vya kibiashara, lakini pia haiogopi vita hivyo, na hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru wa bidhaa itailazimisha China kuchukua hatua za lazima za kuijibu.

    akizungumzia amri iliyotolewa hivi karibuni na Marekani kuhusu kuziwekea vizuizi vya kibiashara kampuni za China ikiwemo Huawei, Bw. Gao amesisitiza kuwa China inapinga kitendo cha kutumia ovyo dhana ya usalama wa nchi na hatua za kudhibiti uuzaji bidhaa nje ya nchi, na pia italinda kithabiti haki halali za kampuni za China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako