• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapanua maeneo ya kupanda soya ili kupunguza uagizaji kutoka nje

    (GMT+08:00) 2019-05-17 10:37:29

    Wakulima wakubwa wa soya nchini China wanafanya juhudi za kuongeza uzalishaji wa soya bora ili kupunguza utegemezi wa nchi hiyo kwa mazao hayo kutoka nje, na inatarajiwa kuwa maeneo ya kupanda soya yatapanuliwa kwa asilimia 10 mwaka huu. Kwa mujibu wa ripoti ya maendeleo ya sekta ya kilimo ya China ya mwaka 2019 iliyotangazwa Jumatatu, uagizaji wa soya nchini China ulishuka kwa mara ya kwanza mwaka jana katika miaka saba iliyopita, na kwa kiwango cha asilimia 7.9. Wakati huohuo, bei za soya kwa mauzo ya baadaye katika Bodi ya Biashara ya Chicago Jumatatu zilishuka hadi kiwango cha chini zaidi katika miaka 10 iliyopita, huku wafanyabiashara wakionyesha wasiwasi wao kwa kupamba moto mgogoro wa kibiashara kati ya Marekani na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako