• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara kati ya China na nchi za nje yadumisha utulivu

    (GMT+08:00) 2019-07-12 20:09:13

    Takwimu zilizotolewa leo na Idara Kuu ya Forodha ya China zinaonesha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje ilifikia karibu dola trilioni 2.14 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 3.9 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo. Wakati uchumi wa dunia unadidimia na vitendo vya kujilinda kibiashara vinaongezeka, ni vigumu kwa China kupata matokeo hayo mazuri katika biashara ya nje.

    Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, maendeleo ya biashara kati ya China na nchi za nje yameonesha mwelekeo wa kudumisha utulivu, na kuongeza sifa.

    Kwanza, biashara hiyo imepata injini mpya. Biashara ya bidhaa zenye faida kubwa zaidi kati ya China na nchi za nje iliongezeka kwa asilimia 5.5, na biashara iliyofanywa na makampuni binafsi ya China iliongezeka kwa asilimia 11.

    Pili, China imeongeza biashara na nchi nyingine baada ya kutokea kwa mvutano wa kibiashara na Marekani. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, biashara kati ya China na Marekani ilipungua kwa asilimia 9, wakati huohuo, biashara kati ya China na Umoja wa Ulaya, Umoja wa Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia na Japan iliongezeka kwa asilimia 11.2, 10.5 na 1.7. Zaidi ya hayo, biashara kati ya China na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" iliongezeka kwa asilimia 5.8.

    Tatu, muundo wa bidhaa zinazouzwa na China katika nchi za nje umeboreshwa zaidi. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, mauzo ya bidhaa za kielektroniki za China haswa magari yanayotumia nishati ya umeme katika nchi za nje yaliongezeka kwa asilimia 5.3.

    Pamoja na Marekani kuchochea mvutano wa kibiashara na China, cha kushangaza ni kwamba, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, mauzo ya bidhaa za China kwa Marekani yalipungua kwa asilimia 2.6, ambapo manunulizi ya China ya bidhaa kutoka Marekani yalipungua kwa asilimia 25.7 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo. Hali hii inaonesha kuwa, nafasi za bidhaa za Marekani katika soko la China inaweza kuchukuliwa na bidhaa za nchi nyingine kwa urahisi zaidi kuliko bidhaa za China katika soko la Marekani. Katika kipindi hicho, pengo la biashara kati ya Marekani na China liliongezeka kwa asilimia 12, na hali halisi imeenda kinyume na matarajio ya Marekani ya kuanzisha mvutano wa kibiashara na China.

    Hivi sasa, biashara ya kimataifa inakabiliwa zaidi na utatanishi. Hata hivyo mwelekeo mzuri ya maendeleo ya biashara kati ya China na nchi za nje haujabadilika, na hali hii inaweka msingi imara wa maendeleo yenye sifa zaidi ya uchumi wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako