• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mageuzi ya shirika la IMF yatakiwa kuendelea kuinua kiwango cha sauti na uwakilishi wa makundi ya kiuchumi yanayojitokeza

    (GMT+08:00) 2019-07-17 19:38:58

    Kamati ya utendaji ya shirika la fedha la kimataifa IMF imetangaza kuwa imekubali ombi la kujiuzulu la mkurugenzi mkuu Bibi Christine Lagarde, na itaanzisha mara moja mchakato wa kumteua mkurugenzi mkuu mpya. Katika kipindi cha ukaguzi mkuu wa 15 wa mgao cha shirika hilo, mrithi wa Bibi Lagarde anatakiwa kufuata mwelekeo wa zama, kuhimiza mageuzi ya mgao na usimamizi ya shirika la IMF, kuendelea kuongeza sauti na uwakilishi wa makundi ya kiuchumi yanayojitokeza na nchi zinazoendelea, ili kulifanya shirika hilo kulinda uhalali na ufanisi wake.

    IMF siku zote inafanya juhudi za kuhimiza ushirikiano wa sarafu wa dunia, kutoa fedha na msaada, kulinda utulivu wa kifedha wa kimataifa. Baada ya kuingia katika karne mpya, utaratibu wa uchumi wa dunia umekuwa na mabadiliko makubwa. Kwa upande fulani, makundi ya kiuchumi yanayojitokeza yanakua kwa haraka, na yanachukua nafasi kubwa zaidi katika uchumi wa dunia na kutoa mchango zaidi kwa ongezeko la uchumi wa dunia. Kwa upande mwingine, mfumo wa usimamizi wa uchumi wa dunia uliopo hivi sasa umekosa nguvu ya kupunguza hali ya uchumi wa dunia isiyo na uwiano, kuhimiza mchakato wa biashara ya pande nyingi na utatuzi wa mgogoro wa madeni ya mamlaka. Katika hali hiyo, kuhimiza mageuzi ya shirika hilo na kuinua ushiriki na sauti za makundi ya kiuchumi yanayojitokeza na nchi zinazoendelea katika mambo ya uchumi wa dunia, umekuwa ni mwelekeo usiozuilika.

    Lakini mgao na usimamizi wa shirika hilo haujaonesha mabadiliko ya utaratibu wa uchumi wa dunia. Kwa mfano, pato la taifa la makundi ya kiuchumi yanayojitokeza na nchi zinazoendelea limefikia nusu ya pato hilo la dunia nzima, ambalo linachangia zaidi ya asilimia 80 ya ongezeko la uchumi wa dunia. Kiwango cha Marekani katika uchumi wa dunia kimepungua hadi kufikia asilimia 20 hivi, lakini Marekani bado ina haki kubwa zaidi ya kupigia kura katika shirika hilo ambayo ni asilimia 16.52, huku ikiwa na haki ya turufu katika maamuzi makubwa. Nchi zilizoendelea bado zina hadhi ya kutawala shirika la IMF.

    Hivi sasa, shirika hilo linafanya ukaguzi mkuu wa 15 wa mgao, na kutarajiwa kufikia makubaliano kuhusu mgao mpya na kurekebisha mgao huo juu ya msingi wa makubaliano hayo. Katika siku za baadaye, bila kujali nani atakayeongoza shirika hilo, ataona kuinua kwa kiwango cha makundi ya kiuchumi yanayojitokeza na nchi zinazoendelea katika uchumi wa dunia, ni mwelekeo usiozuilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako