• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatoa wito kwa mafungamano ya Afrika ili kutoa nafasi za ajira kwa vijana

    (GMT+08:00) 2019-07-18 09:32:51

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametoa wito kwa serikali za Afrika kukuza mafungamano katika bara hilo ili kustawisha uchumi na kutoa nafasi zaidi za ajira kwa vijana.

    Rais Kenyatta amesema juhudi zote katika kuongeza mafungamano ya Afrika na biashara ndani ya bara hilo zinatakiwa kulenga kutoa ajira zenye heshima na mishahara mikubwa kwa mamilioni ya vijana barani Afrika.

    Pia amesema, wakati Afrika ikielekea kuwa eneo lisilo na mipaka chini ya kuanzishwa kwa Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) lililozinduliwa hivi karibuni, wafanyabiashara wanatarajia sana kunufaika na biashara ambayo si kama tu ina masoko makubwa bali pia fursa kwa maendeleo ya kasi na uvumbuzi na teknolojia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako