• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema maambukizi ya Ebola nchini DRC ni hali ya dharura inayofuatiliwa na jamii ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2019-07-18 09:33:17

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameutangaza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC kuwa hali ya dharura ya afya ya umma kwa jamii ya kimataifa, PHEIC.

    Tangazo hilo limetolewa baada ya mkutano wa kamati ya dharura ya utaratibu wa afya ya kimataifa kuhusu ugonjwa wa Ebola nchini DRC, ikiwa ni mara ya nne kwa nchi hiyo kukumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo tangu Agosti Mosi mwaka jana.

    Habari nyingine zinasema, taarifa ya pamoja inayotolewa na wizara ya afya ya Uganda na WHO zinasema kuwa, mtu mmoja kutoka DRC ambaye alikwenda Uganda kufanya biashara ya samaki, amethibitishwa kufariki dunia kutokana na Ebola.

    Kwa sasa kikundi cha ufuatiliaji kinawatambua na kuwafuatilia watu wote waliowasiliana na mtu huyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako