• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya unga wa mahindi nchini Kenya kuendelea kuwa juu

    (GMT+08:00) 2019-07-18 09:45:12

    Huenda wakenya wakaendelea kununua unga wa Ugali kwa bei ya juu kama ilivyo sasa hadi mwishoni mwa mwaka. Hii ni baada ya waziri Kiunjuri kusema kuwa huenda serikali ikakosa kuagizia mahindi kama ilivyokuwa imepanga hapo awali. Hata hivyo, wakulima wa mahindi nchini Kenya wamepinga madai ya serikali kwamaba kuna upungufu wa mahindi. Wanataka serikali kununua mahindi kutoka kwa wakulima.

    Kamati ya kilimo nchini Kenya ilipata nafasi ya kukutana na Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri, na kulalamikia hatua ya serikali kutaka kuagiza mahindi kutoka nje ya nchi. Huenda shinikizo kutoka kwa kamati hiyo limemlazimu Waziri huyo kusitisha pendekezo la kuagiza mahindi kutoka nje. Hii huenda ikawa nafuu kwa wakulima wa mahindi ila ukawa mwanzo wa mahangaiko kwa wakenya wanaopenda ugal, kwani huenda bei ya unga wa ugali ikapanda zaidi ya ilivyo hivi sasa kabla ya mwezi Oktoba, wakati ambapo wakulima huanza kuvuna mahindi.

    Kulingana na Waziri Kiunjuri, mpango wa kuagiza mahindi kutoka nje ya nchi hauwezekani kwa sasa, kwani muda wa kufanya hivyo umepita, na kama yataagizwa sasa, mahindi hayo yatafika Kenya mwezi Septemba. Hatua hii ilipokelewa vyema na wakulima wa mahindi, ambao sasa wanataka serikali kununua mahindi yao, ila kwa masharti. Hata hivyo, waziri anakisia kwamba huenda hatua hii ikasababisha bei ya unga wa ugali kupanda kwani bado kuna upungufu wa mahindi.

    Gharama ya unga wa ugali kwa pakiti ya kilo mbili imepanda kutoka shilingi tisini na shilingi mia moja mwezi Mei mwaka huu, na kuuzwa kati ya shilingi 115 na 120 mwezi Julai. Takwimu kutoka kutoka wizara ya Kilimo zinaonyesha kwamba, kila mwezi Kenya hushuhudia upungufu wa mahindi wa kati ya magunia laki nane na milioni moja, jambo ambalo wakulima wa mahindi wanasema si kweli.

    Kwa sasa wapenzi wa ugali watalazimika kugharamika zaidi huku wakulima wakiomba serikali kubuni mikakati ya kuzuia hali kaa hii na kuwapa kipao mbele wakulima wa humu nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako