• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Awamu ya pili ya mafunzo ya wakunga wasaidizi wa Afrika wafanyika China

    (GMT+08:00) 2019-07-18 15:11:56

    Uzinduzi wa awamu ya pili ya mafunzo ya wakunga wasaidizi wa Afrika "Angel of Life" umefanyika tarehe 16 Julai, katika chuo kikuu cha matibabu cha Wenzhou, mkoa wa Zhejiang.

    Mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa wiki mbili, ambapo wanafunzi 25 kutoka Ghana, Uganda, Rwanda, Nigeria na Zambia watapata mafunzo.

    Mradi huo ulianza rasmi tarehe 20 Agosti mwaka jana, kwa lengo la kutoa mafunzo ya ustadi wa ukunga kwa wanafunzi wa Afrika wanaosomea udaktari nchini China, kutoa ujuzi wa afya ya wanawake na watoto kwa vijana wa Afrika, ili kuboresha kiwango cha afya cha wajawazito, wanaojifungua, na watoto wachanga barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako