• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazidi kuimarisha kwa pande zote ulinzi wa hakimiliki za ujuzi

    (GMT+08:00) 2019-07-18 17:07:48

    Mkutano wa kawaida wa baraza la serikali ya China umetoa mipango ya kuzidi kuimarisha kazi za kuhifadhi hakimiliki za ujuzi na kulinda kihalisi maslahi halali za mashirika na wadau mbalimbali wa soko. Watalaamu wengi wamesema, nguvu ya ulinzi wa hakimiliki za ujuzi ya China inaendelea kuongezeka, ambayo itasaidia kuboresha mazingira ya kibiashara, kuhimiza uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

    Takwimu zinaonesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, kesi 6529 za ukiukaji wa hakimiliki za ujuzi na kesi elfu 11.5 za alama haramu za biashara zimechunguzwa. Kupitia hatua mbalimbali ikiwemo kutekeleza operesheni maalumu za utekelezaji wa sheria, kuhimiza ujenzi wa mfumo wa kulinda hakimiliki za ujuzi, kuimarisha uwezo wa timu za ulinzi wa hakimiliki za ujuzi za kimitaa na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa wa ulinzi wa hakimiliki za ujuzi, nguvu ya ulinzi wa hakimiliki za ujuzi ya China inaendelea kuongezeka. Mjumbe wa kamati maalumu ya sheria ya alama za biashara na sheria ya ushindani ya taasisi ya hakimiliki ya ujuzi ya Beijing Bw. Yang Jiangan anasema,

    "Kwa ujumla, naona kuimarisha ulinzi wa hakimiliki za ujuzi sio tu ni mahitaji ya ushirikiano na mawasiliano ya kimataifa, bali pia ni mahitaji ya maendeleo yetu. Kwa sababu maendeleo ya uchumi wetu yamebadilika kutoka kipindi cha maendeleo ya kasi ya juu hadi kipindi cha maendeleo ya sifa ya juu, ambayo yako katika kipindi muhimu cha mabadiliko ya mtindo wa maendeleo na mabadiliko ya nguvu ya kuhimiza ukuaji. Hivyo tunatakiwa kuchochea uvumbuzi kama injini ya kwanza, na kuchukua njia ya kuhimiza maendeleo kwa uvumbuzi. Kuimarisha ulinzi wa hakimiliki za ujuzi ni mambo muhimu ya kukamilisha mfumo wa ulinzi wa hakimiliki, ambayo pia ni uchochezi mkubwa wa kuinua ushindani wa China."

    Kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na idara ya hakimiliki za ujuzi ya China, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu idadi ya maombi ya hakimiliki za ujuzi za uvumbuzi yaliyotolewa na wageni nchini China imefikia elfu 78, ambayo inaongezeka kwa asilimia 8.6 kwa kulinganishwa na ya mwaka jana, huku idadi za maombi ya alama za biashara yaliyotolewa na wageni nchini China ikifikia laki 1.27 ambayo inaongezeka kwa asilimia 15.4 ikilinganishwa na ya mwaka jana. Ongezeko la kudumu la idadi za maombi ya hakimiliki za ujuzi za uvumbuzi na alama za biashara yaliyotolewa na wageni nchini China limeonesha imani jumuiya ya kimataifa kwa ulinzi wa hakimiliki za ujuzi nchini China.

    Mkutano wa kawaida wa baraza la serikali ya China hivi karibuni umesema, China itaendelea kuimarisha utekelezaji wa sheria wa hakimiliki za ujuzi, na kuchukulia kwa usawa maslahi halali ya mashirika na wadau mbalimbali wa soko. Profesa Cui Fan kutoka chuo cha uchumi na biashara ya kimataifa cha Chuo Kikuu cha Uchumi na Biashara kwa Nje UIBE amesema, hatua hiyo inafuata kanuni husika za shirika la biashara la dunia WTO. Anasema,

    "Tukizungumzia ulinzi usio na upendeleo wowote, tunatakiwa kulinda mashirika ya ndani na kampuni zinazowekezwa na wafanya biashara wa kigeni, huku tukilinda hakimiliki za ujuzi za bidhaa za kampuni za kigeni zinazouzwa nchini China. Kwa mujibu wa makubaliano yanayohusiana na hakimiliki za ujuzi ya shirika la WTO, kanuni za msingi za ulinzi huo ni kuwachukulia kama raia. Hivyo kigezo cha ulinzi cha sheria yetu kinafuata kanuni husika za shirika la WTO."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako