• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 7-Septemba 13)

    (GMT+08:00) 2019-09-20 18:20:36
    Nigeria yaanza kuondoshwa raia wake kutoka Afrika Kusini

    Nigeria imeanza zoezi la kuwaondoa raia wake waishio nchini Afrika Kusini, ambao wameoredheshwa kwenye ubalozi wa nchi hiyo nchini Afrika Kusini. Watu 640 ndio wanatarajiwa kusafirishwa kutoka Johannesburg kwenga Nigeria.

    Kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nchi za nje ya Nigeria kwenye ukurasa wake wa twitter inakadiriwa kuwa idadi ya raia 313 watachukuliwa kutoka Afrika Kusini katika awamu ya kwanza na waliosalia watasafirishwa siku za Alhamisi na Ijumaa wiki hii.

    Serikali ya Nigeria tayari iliwaonya raia wake waliopo Afrika Kusini wasisafiri ama kuelekea kwenye maeneo ambayo ghasia hizo zimeshamiri mpaka pale hali itakapotengemaa.

    Wizara ya mambo ya Nje ya Nigeria ilisema mmliliki wa Shirika la Ndege la Air Peace yupo tayari kuwasafirisha bure wale wote watakaotaka siku ya Ijumaa.

    Awali waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama aliwaambia wanahabari siku ya Jumatano wiki iliyopita kuwa kulingana na taarifa zilizowafikia, hakuna raia wa Nigeria aliyepoteza uhai kwenye ghasia zinazoendelea.

    Rais Muhammadu Buhari alisema kuwa anamtuma mwakilishi wake kwenda Afrika Kusini kueleza 'ghadhabu' zao juu vurugu zinazoendelea.

    Hatua hiyo inakuja wakati uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeanza kuwa mzuri, baada ya kukumbwa hali ya sintofahamu kwa wiki moja iliyopita .


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako