• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uingereza kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa kamati ya EU kuhusu Brexit

    (GMT+08:00) 2019-09-14 18:41:34

    Msemaji wa ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza amesema waziri mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson atafanya mazungumzo na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jean-Claud Juncker nchini Luxembourg kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya. Hii ni mara ya kwanza kwa Bw. Johnson kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Bw. Junker tangu aingie madarakani.

    Msemaji huyo amesema mazungumzo hayo ni sehemu ya juhudi za Uingereza kutafuta njia ya kufikia makubaliano kabla ya tarehe 31 mwezi Oktoba. Pande hizo mbili zinafanya majadiliano na kufanya juhudi kufikia makubaliano lakini bado zinakabiliana na matatizo mengi.

    Bw. Johnson amewahi kusema mara nyingi ataiongoza Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya tarehe 31 mwezi Oktoba bila kujali kama kuna makubaliano au la, na hataomba kuahirisha mpango wa kujitoa Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako