• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini awaomba radhi wazimbabwe na waafrika wengine kufuatia mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni

    (GMT+08:00) 2019-09-15 17:21:58

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema serikali inajitahidi kufanya kazi ili kukomesha mashambulizi yanayotokana na chuki dhidi ya wageni.

    Akiongea kwenye shughuli ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Bw. Robert Mugabe, Rais Ramaphosa amesema waafrika kusini hawana chuki dhidi ya wageni na ameomba radhi kwa wazimbabwe na waafrika wengine, kutokana na vurugu zilizotokana na chuki dhidi ya wageni zilizosababisha vifo vya watu 12 ikiwa ni pamoja na wazimbabwe wawili, na kuwafanya wengine wengi kukimbia makazi yao.

    Amesema kilichotokea nchini Afrika Kusini ni kinyume na kanuni ya umoja kati ya waafrika ambayo ilipiganiwa na marehemu Mugabe, marehemu Nelson Mandela na viongozi wengine wa mapinduzi wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako