• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa rais wa China ahudhuria shughuli ya mazishi ya Mugabe

    (GMT+08:00) 2019-09-15 17:22:48

    Mjumbe maalumu wa rais wa China, ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya kisiasa la China Bw. Gu Shengzu, amehudhuria shughuli ya mazishi ya aliyekuwa rais wa Zimbabwe Bw. Robert Mugabe.

    Kwa niaba ya rais Xi Jinping, serikali na wananchi wa China, Bw. Gu ametoa rambirambi kutokana na kifo cha Bw. Mugabe, na kuwapa mkono wa pole rais Emmerson Mnangagwa, wananchi wa Zimbabwe na jamaa wa Bw. Mugabe.

    Alipokuwa nchini Zimbabwe, Bw. Gu pia amekutana na rais Mnangagwa, na kusema Bw. Mugabe ni mwanasiasa hodari wa Zimbabwe na Afrika, na kiongozi wa ukombozi wa taifa la Zimbabwe, na pia alitoa mchango muhimu kwa ajili ya kuhimiza urafiki kati ya China na Zimbabwe, na China na Afrika. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Zimbabwe, na kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kuendelea kwa mfululizo.

    Naye rais Mnangagwa amesema rais Xi kutuma mjumbe maalumu kuhudhuria shughuli za mazishi ya Bw. Mugabe kumeonesha urafiki mkubwa kati ya watu wa nchi hizo mbili, na Zimbabwe inapenda kuendelea kuimarisha na kuendeleza ushirikiano wa kirafiki kati yake na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako