• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ikulu ya Iraq yahitimisha rasimu ya sheria mpya ya uchaguzi wakati wa maandamano ya kitaifa

    (GMT+08:00) 2019-11-12 09:32:42

    Shirika la habari la serikali ya Iraq INA limeripoti kuwa, ikulu ya Iraq imehitimisha rasimu ya sheria mpya ya uchaguzi kutokana na msaada wa wataalamu wa Iraq na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa rasimu hiyo, tume mpya ya uchaguzi itaundwa na mahakama ya Iraq na wataalamu wengine badala ya kufuata mfumo wa mgao wa vyama vya kisiasa. rasimu hiyo pia itapunguza idadi ya viti vya bunge kwa asilimia 30, na kushusha ukomo wa chini wa umri wa wawakilishi kuwa miaka 25.

    Baraza la mawaziri la Iraq pia limewasilisha rasimu yake ya sheria ya uchaguzi, majadiliano yanaendelea kuunganisha rasimu hizo mbili kuwa moja ya mwisho, ambayo itawasilishwa bungeni ili ipitishwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako