• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa meli mpya ya kisasa Ziwa Victoria kukamilika 2021

    (GMT+08:00) 2019-11-12 19:04:58
    Ujenzi wa meli mpya ya kisasa ziwa Victoria umefikia asilimia 35.

    Hadi kukamilika kwake,ujenzi huo unatarajiwa TSh bilioni 86.

    Hayo yameelezwa juzi jijini Mwanza na Kaimu Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (Mscl) Mwanza,Abel gwanafyo,kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa huduma hizo.

    Gwanafyo alisema meli hiyo ina uwezo wa tani 400 yakiwamo magari madogo 20 na makubwa matatu na kubeba abiria 1,200 .

    Aidha alisema meli hiyo itakuwa ya kisasa kuliko meli zingine katika Ziwa Victoria.

    Ujenzi wa meli hiyo ulianza mwaka 2018 na unatarajiwa kukamilika 2021.

    Meli hiyo inajengwa na kampuni ya GAS EntecCo Ltd kwa kuungana na Kang Nam Cooperation ya Korea Kusini pamoja na SUMA JKT ya Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako