• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe: Utoaji pesa katika akaunti za benki kuanza leo

    (GMT+08:00) 2019-11-12 19:05:41
    Benki za biashara nchini Zimbabwe zimekusanya noti mpya za $30 milioni jana kutoka Benki Kuu ya Zimbabwe (RBZ) na wenye akaunti wataweza kutoa $300 kila wiki kutoka benki za biashara katika ugavi wa utoaji pesa unaoanza kutekelezwa leo.

    Takriban wamiliki wa akaunti za benki 100,000 wataweza kutoa pesa wiki hii,labda kuwe na agizo jingine kutoka Benki kuu ya Zimbabwe.

    Gavana wa Benki Kuu ya Zimbabwe Dkt John Mangudya alisema hatua zimechukuliwa kuhakikisha pesa hizo hazitolewi benki na kuingizwa kwenye soko lisilo rasmi la pesa.

    Dkt Mangudya alisema anatarajia benki zote kuanza kutoa noti mpya na sarafu hii leo.

    Huku viwango vya utoaji pesa vikiwa ni $300 kwa wiki,mamlaka zinalenga kupitia upya viwango hivyo wakati ambapo hali itaimarika,katika juhudi za kurejesha usawa katika uchumi.

    Benki pia zinatarajiwa kuanza kuweka pesa katika mitambo ya ATM hivi karibuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako