• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mvua kubwa zaathiri watu 170,000 nchini Jamhuri ya Congo

    (GMT+08:00) 2020-01-24 17:00:28

    Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema mvua kubwa zilizonyesha katika miezi minne iliyopita zimeathiri watu 170,000 nchini Jamhuri ya Congo.

    Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Bw. Haq amesema wahanga ni pamoja na wakimbizi elfu tatu kutoka nchi jirani, na kwamba mashamba yenye kilomita za mraba zaidi ya 63 yameharibiwa. Mvua inaendelea kunyesha katika badhi ya maeneo ya nchi yaliyoko chini ya ikweta, na kupelekea hofu ya kuongezeka kwa mafuriko, watu kukosa makazi na hatari kubwa ya magonjwa yanayosababishwa na maji.

    Aidha amebainihsa kuwa ili kukabiliana na hali ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa na washirika wake wanasaidia timu ya mwitikio inayoongozwa na serikali kwa kutoa chakula, vitu visivyo chakula, makazi, maji, pamoja na usafi, ambapo watu zaidi ya 80,000 wamepata msaada wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako