• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema mlipuko wa virusi vya Korona nchini China bado haujawa dharura ya afya duniani

    (GMT+08:00) 2020-01-24 17:29:06

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema ni mapema kutangaza mlipuko wa virusi vya Korona vinavyosababisha nimonia nchini China kuwa ni tukio la dharura ya afya ya umma duniani, huku likitahadharisha kuwa idadi ya wagonjwa inaweza kuongezeka wakati ambapo virusi bado havijajulikana.

    Akiongea na wanahabari baada ya mkutano wa faragha wa Kamati ya Dharura, mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema hii ni dharura ya China, lakini bado haijawa dharura ya afya ya duniani.

    Hapa nchini China, wizara ya Sayansi na Teknolojia imetangaza kuwa timu ya watafiti yenye wataalamu 14 imeundwa ili kusaidia kuzuia na kudhibiti mlipuko wa virusi vya korona. Timu hiyo ni sehemu ya mradi wa dharura wa sayansi na teknolojia ambao umezinduliwa kwa pamoja na Kamati ya Afya ya Taifa na idara nyingine katika mkutano wa hivi karibuni. Mradi huo utatoa uungaji mkono wa sayansi na teknolojia katika vipengele 10 vya utafiti, vikiwemo, kufuatilia virusi, usambazaji wa virusi, njia za ugunduzi, mabadiliko ya jeni na kuendeleza chanjo.

    Wakati huohuo mji uliopo katikati ya China wa Wuhan utafuata mfano wa matibabu ya SARS wa Beijing na kujenga hospitali maalumu za kulaza wagonjwa walioathirika na mlipuko wa nimonia unaosababishwa na virusi vya korona. Kulingana na makao makuu ya kudhibiti na kutibu ugonjwa huo ya Wuhan, hospitali hiyo itakuwa na eneo la mita za mraba 25,000 na itaanza kutumia Februari 3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako