• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China iko tayari kuisaidia Marekani kupambana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-27 17:21:35

    Rais Xi Jinping wa China amesema anafuatilia sana na kutia wasiwasi na hali ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Marekani, na kusema China iko tayari kuisaidia Marekani kukabiliana na virusi hivyo kadri ya uwezo wake.

    Rais Xi amesema hayo leo alipoongea kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani Donald Trump. Akitoa wito kwa China na Marekani kupambana na virusi vya Corona kwa pamoja, Rais Xi amesema China inapenda kuendelea kutoa taarifa na uzoefu wake kwa Marekani kuhusiana na virusi hivyo bila kuficha. Pia ameitaka Marekani ichukue hatua halisi kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, kuongeza ushirikiano katika kudhibiti maambukizi hayo na sekta nyingine, na kukuza uhusiano usio wa kupambana na kukabiliana, na badala yake kuheshimiana, kushirikiana na kutafuta mafanikio ya pamoja.

    Kwa upande wake, rais Trump amesema yeye na viongozi wa nchi nyingine wamepongeza maoni na mapendekezo yaliyotolewa na rais Xi kwenye mkutano maalum wa kundi la G20 kuhusu virusi vya Corona uliofanyika jana. Amesema ameelimishwa na uzoefu wa China katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, na kuahidi kuwa atajituma kuhakikisha Marekani na China zinaondoa tofauti na kujizatiti katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona. Pia ameishukuru China kwa kutoa vifaa vya matibabu kwa Marekani.

    Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha John Hopkins, Marekani imeipiku China na kuwa nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na kesi nyingi zaidi za maambukizi ya virusi vya Corona, ambapo mpaka jana mchana kwa saa za huko, kulikuwa na kesi 85,653, na watu 1,290 wamefariki kutokana na maambukizi hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako